Kisutu vurugu!
2008-12-16 19:06:13
Na Mwandishi Wetu, Kisutu
Eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana palikuwa hapatoshi! Watoto wa mjini wanasema, ilikuwa vurugu tupu! Ulinzi mkali wa askari wenye mitutu ya bunduki walioambatana na mijibwa mikali, (kama inavyoonekana pichani ukurasa wa mbele) ulifanya eneo hilo liwe kama uwanja wa mapambano.
Watu waliofika mahakamani hapo jana walishuhudia askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Polisi wakila mingo nje ya mahakama kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kabla na baada ya kufikishwa kortini kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.
Mahuhuda wameiambia Alasiri kuwa hali hiyo iliwatisha na kuwasababishia hofu kubwa kiasi cha kuona ulinzi huo kuwa ni kama vurugu badala ya amani.
Askari karibu 50 wa Jeshi la Magereza na Polisi jana walifurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuhakikisha kuwa kunakuwa na amani na utulivu wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Mgonja alipoburuzwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kutumia madaraka yake vibaya.
Licha mtuhumiwa kufikishwa mchana, lakini ulinzi ulianza tangu asubuhi.
Alifikishwa mishale ya saa 7:20 mchana akiwa kwenye gari aina ya Toyota Rav4 lenye namba za usajili T 123 ATW na kupandishwa kizimbani mishale ya saa 8:15 mchana.
No comments:
Post a Comment