Friday, February 5, 2010

BIOGRAPHY OF PROF.JUSTINIAN RWEYEMAMU

VIVA LE TANZANIA
Project: Biography of Prof. Justinian Rweyemamu
Profesa Justinian Rweyemamu

Ninakumbuka vizuri sana jinsi wanazuoni tulivyostuliwa na kifo cha ghafla cha mmoja ya wachumi wakwanza Tanzania, Prof. Justinian Rweyemamu mnamo mwaka 1982, akiwa na umri wa miaka 40.
Katika umri wake mdogo aliweza kufanya mengi kwa kutumia kipaji chake kwa ajili ya nchi yake na nchi maskini duniani. Katika kipindi hicho marehemu alifanikiwa:
1) kupata PhD ya Uchumi (Harvard),
2) kuandika vitabu kadhaa mashuhuri kuhusu historia na muelekeo wa uchumi wa Tanzania,
3) kuwa mhadhiri na mkuu wa idara ya Uchumi wa kwanza mzawa hapa UDSM, 4) kuwa katibu mkuu Wizara ya Mipango,
5) kuwa Mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya Uchumi,
6) Mjumbe wa sekretarieti ya "Committe for Development Planning", Umoja wa Mataifa, n.k.
Alikuwa mcheshi, msikivu, na mwenye upeo wa hali ya juu katika kuchanganua masuala ya Uchumi na Falsafa. Je watanzania, mnamkumbuka msomi huyu?
Nipo katika mchakato wa kuandika biography ya Prof. Rweyemamu, na ningeomba yeyote mwenye kumbukumbu muhimu tuwasiliane kupitia anuani: mfaume.abdalla@gmail.com

kwa wasifu tembelea:
http://en.wikipedia.org/wiki/Justinian_Rweyemamu

asante

No comments: