Friday, February 5, 2010

VIMWANA WAPYA WA REDDS

VIVA LE TANZANIA
mwali mpya wa redds afichuliwa usiku huu dar
Bosi wa Masoko wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), David Minja akizungumza usiku wa kuamkia leo katika kiota cha maraha cha Savannah Lounge cha Paradise City hotel jijini Dar wakati wa uzinduzi wa chupa mpya ya Redds. Kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Redds Kabula Nshimo.

Kiongozi wa Bendi ya Machozi, Judidh Wambura
‘’Lady JD akiimba na msanii wa baendi hiyo Choniko Furaha

Hashim Lundenga akimmwagia sifa zake mwali
mpya akiwa anakula konozzz na MC wa shughuli Joketi
kilaji cha redds premium lager kimekuja na muonekano mpya kwenye uzinduzi mahususi uliofanyika usiku huu kwenye mnuso wa nguvu ulioandaliwa na TBL kwenye kiota cha maraha cha savannah lounge kilichopo ndani ya hoteli bomba ya Paradise City ghorofa ya tatu ya jengo la benjami william mkapa towers mtaa wa azikiwe avenue jijini dar na kuhudhuriwa na mamia ya wadau ambao wameonesha kufurahia muonekano mpya wa mwali huyu
bosi wa masoko wa TBL David Minja (shoto) akiwa na meneja wa Kilimanjaro lager George Kavishe (kuume) na meneja wa Safari lager Fimbo Butala (pili kuume) na mdau wakifurahia sherehe za kumfichua mwali redds usiku huu katika savannah lounge
Miss Tanzania 2009 Miriam akiwa na wenzie kwenye uzinduzi huo

Lady Jaydee na Machozi band walikuwapo kutumbuiza
meneja wa redds kabula (shoto) akiongoza jive
savannah lounge palikuwa hapatoshi
ankal na mikonozzz walikuwepo na mama wa mitindo asia idarous (kuume) na khadija mwanamboka pamoja na wabunifu mahiri wa kiume
savannah lounge hakika palipendeza
sio chupa tuu hata kopo limekuja kuwashika kivingine....





No comments: