Tuesday, December 16, 2008

KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NAE KEKO

VIVA LE TANZANIA
BREKING NYUUUZZZZZZZZZZ
gray mgonja akiwa mahakami kisutu leo kabla ya kusomewa mashataka yake sasa hivi. chini akiingia chumba cha mahakama akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi na magereza
KATIBU MKUU WA ZAMANI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO GRAY MGONJA AMETINGA KIZIMBANI SASA HIVI KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA KISUTU HAPA DAR KUJIBU MASHTAKA MBALIMBALI.
MGONJA ANAKABILIWA NA SHTAKA LA KUITIA HASARA SERIKALI YA BILIONI 11 PAMOJA NA KUTUMIA VIBAYA MADARAKA YAKE.
MGONJA ANATARAJIWA KUUNGANISHWA NA MAWAZIRI WA ZAMANI BASIL MRAMBA NA DANIEL YONA KATIKA KESI YAO.
AMEWEKWA RUMANDE HADI KESI YAKE ITAPOTAJWA TENA DECEMBER 29, 2008 BAADA YA KUSHINDWA KUTIMIZA MASHARTI MAGUMU YA DHAMANA IKIWA NI PAMOJA NA SHILINGI BILONI 5.9 NA WADHAMINI WAWILI PAMOJA NA KUSALIMISHA HATI YA SAFARI NA KUTOTOKA NJE YA DAR.

No comments: