Friday, December 12, 2008

TID NEEMA

TID asamehewa na JK



Msanii wa muziki wa kizazi nchini Khalid Mohammed ‘maarufu kama TID’ aliyekuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja katika gereza la Segerea, ameachiwa huru kupitia msamaha kwa wafungwa uliotolewa na Rais Kikwete

TID ambaye Julai 23, mwaka huu alihukumiwa katika mahakama ya Kinondoni kutokana na kujeruhi, alikuwa ni mmoja ya wafungwa 4,306, walionufaika na msamaha huo ambao ni kwa mujibu wa Ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kutokana na kuachiwa huru huko kwa TID, mashabiki wa msanii huyo jana walikuwa katika furaha za aina yake kwa kupita katika maeneo ya Kinondoni yalipo makazi ya msanii kuyo na kushangilia huku baadhi yao wakiwa wamevua mashati.

TID alirejea nyumbani kwake akiwa ndani ya gari aina ya Pajero, akisindikizwa na magari kadhaa alionekana ni mpole na mtulivu tofauti na alivyozoeleka kabla ya kukumbwa na kifungo hicho.

No comments: