Friday, December 12, 2008

BURIANI MUKEBA

Nyota iliyoacha majonzi Afrika Kusini

Miriam Makeba alizaliwa tarehe 4 Machi 1932 ndani ya jiji la Johannesburg huko Afrika Kusini.



Alianza kazi ya muziki mwanzoni mwa 1950 akiwa na kundi la The Skylarks, baadaye alijiunga na kundi la Manhattan Brothers, kwani makundi hayo yalikuwa yakipiga muziki wa Jazz wenye vionjo vya Kiafrika kusini.

Mwaka 1959 alianza kutambulika kimataifa wakati wa ziara yake nchini Marekani akiwa na kundi la muziki la Afrika Kusini la Manhattan Brothers.

Mama yake ni wa kabila la Swazi sangoma na Baba yake ni wa kabila la Xhosa, kwani Baba yake Miriam alifariki wakati Miriam akiwa na umri wa miaka sita.

Miriam alikuwa ni mwanamuziki pekee wakati huo na aliweza kufanikiwa kuzieneza nyimbo zenye asili ya Kiafrika.

Na alikuwa ni miongoni mwa wanamuziki waasisi wa kuchanganya mitindo tofauti ya muziki, na kutengeneza muziki wa kuvutia kama Kwaito.

Mwaka 1959, Miriam alifanya onyesho kubwa pamoja na Hugh Masekela, mume wake wa baadaye. Maonyesho aliyofanya pamoja na albamu nzuri alizorekodi lakini havikumpatia faida.

Baadaye aliamua kufanya matamasha katika nchi za Ulaya na Amerika. Na ulipoanza mkakati wa kupinga Ubaguzi wa rangi uliyokuwa ukiendelea Afrika ya kusini Miriam aliamua kurudi nyumbani kupigania uhuru.

Na baadaye alialikwa Italia katika tamasha la filamu la Venice, kati ya nyimbo za Miriam zilizo maarufu ni Patapata (kwa lugha ya KiXhosa ni "Qongaqothwan").

Wimbo maarufu wa Malaika uliotungwa na Fadhili William Miriam aliuimba akishirikiana na Harry Belafonte, na alirudi tena nyumbani mwaka 1990 na mwaka 1992 alicheza filamu ya sarafina.

Mwaka 2001 aliweza kutunukiwa tuzo ya dhahabu iliyoitwa Otto HMwaka 1959, Miriam alifanya onyesho kubwa pamoja na Hugh Masekela, mume wake wa baadaye. Alifanya maonyesho katika nchi zote alizotembelea mwaka 1992 alicheza filamu ya sarafina.

Mwaka wa 2005, Miriam alifanya ziara ya kimuziki kwa ajili ya kuwaaga marafiki wake wote duniani, iliyomchukua miezi kumi na minne.

Pia alishika nafasi ya 38 ya wanamuziki bora kati ya mia moja waliopewa tuzo nchini Afrika ya kusini.

Alifanya maonyesho katika nchi zote alizotembelea wakati alipokuwa akifanya kazi ya muziki.

Na aliaga dunia kwa shtuko la moyo alfajiri ya tarehe 10 Novemba, 2008, nchini Italia baada ya kutoa onyesho la muziki.

Daima tutakukumbuka, Mungu ailaze Roho ya Miriam Makeba mahali pema peponi.Amina.VIVA LE TANZANIA

No comments: