Tuesday, December 16, 2008

UCHAGUZI TFF

VIVA LE TANZANIA
veterani wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa tff
baadhi ya wchezaji nyota wa zamani wakisubiria matokeo ya uchaguzi wa tff muda huu hapa nssf waterfront, dar. kwa haraka haraka shoto ni jenerali juma mkambi, wa kwanza kulia ni aboubakar salum 'sure boy' akifuatiwa na omar gumbo, john tegete, omar hussein 'keegan' shaaban katwila, mwenye chunlai nyeupe ni abbasi kuka. wadau wenye majina ya wengine tunaomba.
hivi sasa wajumbe ndio wanahojiwa ili wapigiwe kura. kura za rais, makamu wa kwanza na wa pili wa rais tayari zimeshapigwa. tunategemea kupata matokeo kabla ya saa kumi ili kuwahi kuwapokea taifa stars wanaotua leo saa kumi na moja eapoti hapa dar.
redio mbao zinasema nanihii ameshinda kwa kura nyingi, mpinzani wake akiwa kaambulia robo tu. nanihii wa tmk redio hizo zinasema kalamba umakamu wa kwanza na ninihii kawa makamu wa pili.

No comments: