Thursday, January 8, 2009

CLUB BILCANAZ NI NOMA

VIVA LE TANZANIA
club billicanas yafunguliwa leo
baada ya kufanyiwa ukarabati na ukarafati wa takriban mwaka mmoja, hatimaye leo jioni club billicanas pamoja na music club yake ya much more iliyomo humo humo inafunguliwa kwa sherehe maalumu. kwa mujibu wa msemaji wa klabu hicho, kuanzia leo itakuwa wazi kila siku jioni hadi majogoo, kuanzia jumatatu hadi jumatatu. kuhusu mchango wa mlangoni amesema kwa ung'eng'e kiingilio kitakuwa cha saizi ya 'serious clubbing people' na kwamba kila atakayeingia hatojutia alichotoa. bila kuwa na haja ya kupigia kampeni, na kwa bahati ya kutembelea klabu mbalimbali kama vile ange noir ya ukweni kampala, florida 2000 (A na B) za kwa watani wa jadi, lusaka by night ya zambia, chez ntemba ya kinshasa, tam tam ya addis ababa, komba disco ya zenji n.k. club billicanas imesimama na ni ya kujivunia katika ukanda huu wa afrika mashariki na kati. sijui kwingineko na nakubali kukosolewa - kwa wataoingia tu.
club billicanas kwa nje ambako maegesho ya magari yamepigwa mkeka wa nguvu na mataa kibao. redio mbao zinasema hapo nje kwa sasa panaitwa billicanas square...
sehemu ya libeneke kwa chini. hizo mbao na maspika yaliyowekwa chini visikutishe. globu ya jamii ilipokuwa inapita vilikuwa zinaondolewa
upstairs
sehemu ya kupasha moto msuli baada ya libeneke

sehemu ya libeneke inavyoonekana toka balkoni. kwa wadau wa toka zamani wa hapo shepu ya billicanas karibu ni ile ile tu, ila imeboreshwa na kuwekwa kila kitu kipya.

sehemu ya kupasha moto msuli katika music bar ya much more
much more pamekucha...
baadhi ya sehemu za music bar ya much more
mitambo ya kisasa inayo-control kila kitu kuanzia viyoyozi, mataa, muziki n.k. imewekwa. wadau kazi kwenu

No comments: