Mashine tiba ya kansa yaibwa Ocean Road
Zaidi ya wagonjwa 170 hawatapata matibabu ya saratani (kansa) katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es salaam baada ya mtambo wa kuendeshea mashine za kuchoma mionzi kuibwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka taasisi hiyo, kuibiwa kwa kifaa hicho kunafanya shughuli nzima ya uchomaji wa mionzi na tiba ya saratani kusimama.
Akielezea tukio hilo, Mkurugenzi wa Ttaasisi hiyo, Dk Twalib Ngoma, alisema kuwa mtambo huo uliibiwa usiku wa kuamkia jana huku kukiwa na takribani wagonjwa 170 wanaohitaji tiba inayotolewa na mitambo hiyo.
Kwa mujibu wa Dk. Ngoma, mtambo huo hapa nchini upo Ocean Road tu.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi linawashikilia watumishi sita kutoka Taasisi hiyo kwa ajili mahojiano zaidi.
Aidha, huduma za tiba ya saratani zitaendelea baada ya kifaa hicho kupatikana au kununuliwa kingine.
Kifaa hicho pamoja na mashine ya mionzi kinagharimu kiasi cha Sh bilioni moja.
No comments:
Post a Comment