msiba mfuko wa bima ya afya
Mtumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bibi Newaho Mbeye amefariki dunia usiku wa kuamkia Jana katika Hospitali ya Misheni Mikocheni alikokimbizwa baada ya kuugua ghafla usiku wa Jana.
Kabla ya kukutwa na umauti, Hayati Newaho alikuwa kitengo cha Huduma za Wateja- sehemu ya mapokezi ambako aliendelea na kazi zake kama kawaida mpaka muda wa kufunga ofisi ulipofika hiyo jana huku akionekana kuwa na afya njema na huku akitekeleza majukumu yake ya kila siku.
Kwa wale waliofika makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, tangu walipokuwa Sukari House hadi walipohamia Kurasini sura ya marehemu Newaho Mbeye sio ngeni kwao. Mipango na maandalizi mengine ikiwemo mazishi vinaendelea na taarifa kamili baada ya mawasiliano kati ya Uongozi wa Mfuko na Familia ya Marehemu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELELE...
AMIN
MOLA AIWEKE PEMA ROHO YA MAREHEMU NEWAHO MBEYE
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
No comments:
Post a Comment