PASTOR MALISA KUHUBIRI DALLAS,TEXAS, JUMAPILI HII
Kwa niaba ya kanisa la Umoja la hapa Dallas,ninayoheshima kuwajulisha watanzania wote kwamba, mtumishi wa Mungu PASTOR MALISA kutoka Tanzania atakuwa mgeni wetu siku ya Jumapili tarehe 6.12.09 (12.6.09) kuanzia saa kumi na moja na nusu jioni.
Mtumishi huyu amekuwa akitumiwa na Mungu sehemu mbali mbali duniani kwa njia ya kipekee kabisa iliyoambatana na ishara na miujiza mingi.Kwa muda mrefu sasa Mungu amekuwa akimtumia huyu mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kuleta uamsho katikati ya watanzania walioko huku Marekani.
Kwa sasa Pastor Malisa anasimamia kanisa huko Minnessota huku akizunguka sehemu mbali mbali ambazo Bwana amemuagiza kufungua watu ambao wamefungwa katika vifungo mbali mbali vya shetani.
Kutokana na umuhimu wa siku hii, ninaomba kila moja atakaesoma tangazo hili amjulishe mwenzake.Mbali ya huduma ya neno la Mungu kutakuwa na maombezi mbali mbali pamoja na ushauri wa kiroho kwa atakaehitaji.
Wako katika kazi ya Bwana
Pastor Abisalom Nasuwa
Mahali;Umoja International Outreach Church
12727 Hillcrest Road,
Dallas,
Texas 75230
Simu: 214 554 7381,682 552 6204
Email:Umojachurch@yahoo.com
Simu: 214 554 7381,682 552 6204
Email:Umojachurch@yahoo.com
No comments:
Post a Comment