Saturday, December 5, 2009

MATAPELI WANABOA BANA

VIVA LE TANZANIA
tapeli mwingine anaswa, wa juzi wote wameachiwa huru
huyu ni mmoja wa wanaosadikiwa kuendesha genge la utapeli linaloingia mtu kwa gia ya kutaka usaidie kupata tenda WFP ya kuuza dawa ya kuhifadhi chakula huko Kigoma, ambapo wadau wengi wameshalizwa.
huyu hapo alipo ni kituo cha polisi ambapo alinaswa baada ya mwanamama aliyemlia milioni 3 awali kumwita ammalizie milioni 2 alizodai zimebaki kabla ya kutoa sample ya hiyo dawa apelekewe supplier ambaye ni mzungu. mtego ukawekwa na alipopokea pesa na kutoa hiyo sampo ambayo ni juisi ya nini sijui akanaswa.
utapeli kama huu wamefanyiwa watu wengi na tayari habari zimezagaa kila mahali lakini inaonesha bado watu wanazidi kulizwa, na wengi zaidi wamepigiwa simu na hao jamaa na kuchomoa kwa kujua wao ni matapeli.
Majuzi mdada mmoja alifanikiwa kuwanasisha polisi matapeli watatu ambao walifikishwa kituo cha oysterbay wakiwa na gari ambalo likaja kugundulika ni la wizi. habari ambazo Globu ya Jamii imezipata ni kwamba hao jamaa watatu wameshaachiwa kwa kile kinachosemekana kukosekana ushahidi. yaani jamaa walidakwa kabla hawajapokea pesa na kutoa hiyo sampo.
wadau wengi wameilalamikia Globu ya Jamii kudai kwamba jeshi la polisi, pamoja na kujua kamchezo hako, lakini linachukulia kama ni masikhara kwani ni takriban miezi sita sasa toka jamaa waanze kucheza kamchezo hako lakini hawajanaswa na genge lao kuvunjwa. wadau wanahoji kulikoni???

mdau uliye mgeni ya utapeli huu

BOFYA HAPA

No comments: