Friday, December 12, 2008

KAZI TU

Baada ya songi,sasa Rufaa!

Baada ya mwishoni mwa wiki kuzindua songi lake jipya liitwalo 'Siwezi' akiwa gerezani,msanii Khalid Mohamed 'TID'.... amekata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela alichohukumiwa mwaka huu.



Rufani hiyo ya msanii huyo ambaye tangu ahukumiwe kifungo hicho amekwishatumikia miezi minne, itaanza kusikilizwa leo na Jaji Robert Makaramba.

TID alihukumiwa kwenda lupango mwaka mmoja kutokana na kutiwa hatiani kwa kosa la kushambulia na kumjeruhi kichwani na mkononi kijana aliyefahamika kwa jina la Ben Mashibe.

Msanii huyo alimjeruhi Mashibe kichwani na mkononi kwa kutumia chombo cha kuwekea majivu ya sigara ‘ash tray’ na alisomewa mashtaka hayo mara ya kwanza Julai 10, mwaka huu mbele ya Hakimu Hamisa Kalombola wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.VIVA LE TANZANIA

No comments: