Saturday, February 25, 2012

daaah

VIVA LE TANZANIA
Kitu ndani ya black

Kwa mashep haya watabakia vichaa tu tena waliolazwa wodini

MICHAEL ALIVYOKUJA BONGO

VIVA LE TANZANIA

http://www.africapoint.net/wp-content/uploads/2009/06/michaelj.jpgNa Walusanga Ndaki
JE, ulikuwa na umri wa miaka mingapi wakati mfalme wa muziki wa Pop wa Marekani, hayati Michael Jackson alipoitembelea Tanzania mwaka 1992 na kufika shule maalum ya watoto yatima na wenye mtindio wa ubongo iliyopo Sinza?
Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani hadi anakufa 2009, alifika nchini akiwa balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Hassan Diria.
Michael Jackson alitua jioni moja uwanja wa ndege wa Dar akiwa amevalia shati la kijani lenye mikono mirefu, suruali nyeusi na kofia nyeusi, akapandishwa kwenye Mercedes iliyompeleka hadi Kilimanjaro Hotel (wakati huo) ambayo baadaye ikawa Kilimanjaro Hotel Kempinsk, sasa ikiitwa Hyatt Regency Dar es Salaam.

http://www.zenjydar.co.uk/2009months/200906/images/michael+jackson+diria.jpgMashabiki waliokuwa na habari walijazana uwanja wa ndege Dar “kumkodolea mimacho” mwanamuziki huyo wakati huo akiwa na umri wa miaka 34 tu, mbali na wale waliomfuata hadi kwenye hoteli hiyo. Wakaungana na wale waliokuwa wakimsubiri hapo kumshangilia kwa mbinja na mayowe ya furaha.
Pia, mashabiki waliokuwa na habari za ujio na ratiba yake, walijitokeza kwa wingi na kumshangaa vilivyo, The Wacko Jacko alipotembelea shule hiyo ya Sinza, kesho yake.
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, alikutana na mkuu wa nchi ambaye wakati huo alikuwa Rais Ali Hassan Mwinyi.
Ndivyo Michael Joseph Jackson alivyofika Tanzania na kushikana mikono na watoto wa Sinza miaka karibu 20 iliyopita!

ISHA MASHAUZI AZIDI KUJA JUU

VIVA LE TANZANIA

Kikosi kizima cha Mashauzi Classic kikifanya mashambulizi jukwaani.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Isha Mashauzi akilikabili jukwaa vilivyo.

Bendi Taarab inayokimbiza mjini, Mashauzi Classic usiku wa kuamkia leo ilikamua kinoma katika ukumbi wa Mashujaa pande za Vingunguti jijini, Dar katika mualiko maalum toka kwa mama mashuhuri mjini anayefahamika kwa jina la mama K.

Baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo wakishereheka kwa raha zao.

MAMBO YA ROSE NDAUKA!!!

VIVA LE TANZANIA

Maliki Bandawe (wa kwanza kushoto) ambaye ndio mtarajiwa wa Rose,Rose Ndauka na Daudi Mponji ambaye ni mkurugenzi wa Jakaya Group wakiwa makini katika usahili huo.

Hapa wakisikiliza kwa makini wasanii waliojitokeza kwenye usahili.

Staa wa filamu za kibongo nchini, Rose Ndauka siku ya Alhamisi alikuwa katika usahili wa kusaka vijana watakaoshughulika na kazi zote zitakazofanywa ndani ya kampuni ya Ndauka Interteiment.
Katika Usahili huo uliofanyika kwenye ofisi yake iliyopo maeneo ya Magomeni Mtaa wa Somanga ulikuwa ukisimamiwa kwa ukaribu zaidi na mchumba wake mtarajiwa Maliki Bandawe.

Mmoja kati ya wasanii waliojitokeza kwenye usahili ambaye aliwafanya majaji hao kushika mdomo.

Maliki Bandawe ambaye ni mmoja wa majaji akijadili jambo na Rose Ndauka.

Baada ya usahili hapa wakijadiliana nani amepita

TUIOMBEE SONGEA!

VIVA LE TANZANIA
Hali bado tete Songea Send to a friend
Saturday, 25 February 2012 08:09

Askari polisi akionyesha karatasi iliyoandikwa maandishi ya kiarabu kwa waandishi wakati wa mkutano na mjini Songea jana, karatasi hiyo pamoja na hirizi zilikutwa kwenye mifuko ya watuhumiwa wa mauaji yanayohusishwa na ushirikina mjini humo. Picha na Joyce Joliga

WENGINE WAWILI WAUAWA, WANAHARAKATI WATAKA RC, DC, IGP WAFUKUZWE KAZI
Waandishi Wetu
HALI katika Mji wa Songea, Ruvuma bado ni tete. Baada ya watu wanne kuuawa na polisi Jumatano iliyopita, watu wengine wawili wameuawa kwa kupigwa na wananchi juzi.Watu hao ambao ni wanaume, walishambuliwa kwa marungu, mawe na mapanga na kufariki dunia baadaye wakiwa kwenye matibabu. Wananchi waliwashambulia baada ya kuwatuhumu kuhusika na vitendo vya mauaji mkoani humo.

Juzi, Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma liliwakamata na kuwaweka mahabusu askari wake wanne wanaotuhumiwa kutumia risasi za moto na kusababisha vifo vya watu wanne Jumatano wiki hii, wakati wananchi waliokuwa wakipinga mauaji dhidi ya wenzao tisa kwa imani za kishirikina walipopambana na polisi. Watu 41 kujeruhiwa.

Fujo za juzi zilitokea katika Mtaa wa Mkuzo, Songea mara baada ya wananchi kuwakamata watu hao wawili ambao walishindwa kujieleza wakati wakihojiwa. Mbao ya hao, pia alikuwepo mwanamke mmoja ambaye alifanikiwa kutoroka.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao walijitetea kuwa wao ni mafundi ujenzi na walikuwa wakimtafuta mtu ambaye hata hivyo, walishindwa kumtaja jina ili awauzie kiwanja. Baada ya kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha, wananchi waliwataka waeleze walipotoka na wameshaua watu wangapi.

Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Mkuzo, John Moyo alisema wananchi hao walifanya fujo hizo kwenye ofisi yake baada ya kuwafikisha.

Moyo alisema wananchi walipowahoji na kuona wakishindwa kujieleza walianza kuwashambulia kwa kuwapiga na kuwajeruhi vibaya.

Baada ya kushindwa kuwadhibiti, alisema alipiga simu polisi ambao walipowasili eneo la tukio walilazimika kuwatawanya wananchi hao kwa mabomu ya kutoa machozi na kuwapeleka watu hao hospitali.

Wakiwa hospitalini, watu hao walifanyiwa upekuzi na kukutwa wakiwa na hirizi moja kubwa rangi nyeusi pamoja na karatasi nyeupe iliyoandikwa kwa lugha ambayo haikuwa rahisi kusomeka.

Walipoulizwa majina yao, mmoja alisema anaitwa Juma na mwenzake ni Gervase. Katika hali iliyoashiria kuwa Gervase hakutaka atajwe, alimuashiria mwenzake kwa kumbana na pingu.

Wakati huo Gervase alikuwa amevimba uso na alionekana kuishiwa nguvu na hali yake kuzidi kuwa mbaya.

RPC, hosipitali
Baadaye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Benedicto Ngaiza alisema Gervase alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu mapokezi na mwenzake Juma pia aliaga dunia saa chache baadaye.

“Haikuwa rahisi kwa watu hao kupona kwani hali zao zilikuwa mbaya sana. Walikuwa wamejeruhiwa vibaya maeneo ya kichwani na vifo vyao vimetokana na kupoteza damu nyingi,” alisema Dk Ngaiza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda amethibitisha kutokea kwa tukio akiwasihi wananchi waache kuchukua sheria mkononi na badala yake watii sheria bila kushurutishwa pindi wanapomuhisi mtu kuwa ni mhalifu.

“Kwa kweli nasikitishwa na kuumizwa sana na matukio yanayoendelea. Naomba wananchi watulie waache kuuana kwani vitendo hivyo ni vya kinyama na ni uvunjifu wa amani. Tunawaomba wasaidiane na polisi ili tuweze kudhibiti au kutokomeza kabisa wimbi hili la mauaji katika mji wetu,” alisema Kamhanda.

Vikao

Kutokana na wasiwasi uliotanda katika Mji wa Songea, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu kwa upande mmoja na Kamanda Kamhanda kwa upande mwingine jana kutwa waliripotiwa kushinda katika vikao tofauti vyenye lengo la kurejesha utulivu.

Mwambungu alikuwa na kikao na waendesha pikipiki maarufu kwa jina la Yeboyebo jana mchana katika Ukumbi wa Klabu ya Songea ambacho kilikuwa kikihamasisha ulinzi shirikishi ili kukomesha mauaji hayo.

“Madreva pikipiki mna mchango mkubwa sana maana abiria wenu walio wengi mnawafahamu vilivyo hivyo ni vyema kama kuna mtu mna wasiwasi naye mkatoa taarifa polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa,” alisema Mwambungu.

Kamhanda kwa upande wake alikuwa na vikao tofauti katika kambi za polisi na mara ya mwisho ilielezwa kwamba alikuwa Ofisi za Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Songea.

Katika hatua nyingine, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Augustine Songea, wamelalamikia milipuko ya mabomu ya juzi jioni kwamba iliwaathiri kwenye mitihani.

Mmoja wa wanafunzi hao, Hofe Seregius alisema milipuko ya mabomu ambayo yalitua jirani na chuo chao na kwamba yaliwafadhaisha kiasi cha kushindwa kuendelea na mitihani ya historia, hivyo wanataka uongozi wa chuo kuwaruhusu kurudia mtihani huo.

Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Donatus Komba alikiri kuwapo kwa taharuki kwa wanafunzi akisema Polisi walitumia nguvu kubwa dhidi ya wananchi.

Wanaharakati waja juu

Mtandao wa Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika (SAHARiNGON) umelaani kitendo cha polisi kuua raia kwa risasi katika maandamano hayo na kumtaka Rais kuwawajibisha Mkuu wa Mkoa Ruvuma na Kamanda wa Polisi wa Mkoa kwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.

Watendaji wengine waliopendekezwa kuwajibishwa ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ruvuma na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Thomas Ole Sabaya na watendaji wakuu wa Manispaa ya Songea.

Akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana, Mratibu wa SAHRiNGON Tawi la Tanzania, Martina Kabisama alisema wahusika hao wameshindwa kutimiza wajibu wao jambo lililosababisha wananchi kuandamana kwa amani na kushambuliwa na polisi.

Alisema taarifa za matukio ya watu kuuawa kwa kile kilichoelezwa ni imani za kishirikina zilianza kujitokeza Novemba mwaka jana na taarifa zilifika polisi na hadi wananchi wanafikia hatua ya kuandamana, wahusika hawakuonekana kuchukua hatua.

“Ni jambo la kushangaza kwa polisi hao kwenda kuvamia maandamano ya amani na kuua raia. Kitendo hicho tunakilaani sababu wananchi waliandamana kwa amani ikiwa ni namna yao ya kupaza sauti baada ya polisi kushindwa kuchukua hatua dhidi ya matukio hayo,” alisema.

Alisema kitendo hicho cha polisi ni kinyume na haki ya kuishi kama ilivyoelekezwa katika Ibara ya 13 ya Katiba ya nchi ya mwaka 1977.

Alisema kitendo hicho pia kimekiuka haki ya mkusanyiko kama inavyoelezwa katika Ibara ya 21 kifungu cha kwanza, haki ya kusikilizwa na kutoa maoni Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema tukio la maandamano na vurugu zilizotokea ni matokeo ya Serikali kushindwa kuchukua hatua kwa wakati tangu mauaji ya raia yaliyohusishwa na imani za kishirikina yalipoanza kutokea Novemba mwaka jana.

Kabisama alishauri viongozi na watendaji serikalini kujenga utamaduni wa kuchukua hatua dhidi ya matukio mbalimbali yanapotokea kabla ya kusababisha athari.

“Kumejengeka tabia ya Serikali kuchukua hatua baada ya migomo na maandamano kutokea. Tumeshuhudia mgomo wa madaktari watu wamekufa ndipo Serikali inachukua hatua na hili la Songea watu wameandamana na kupoteza maisha ndipo Serikali inachukua hatua. Kitendo hiki cha kushindwa kuchukua hatua kwa wakati ndicho kinacho sababisha wananchi kuchukua sheria mkononi,” alisema.

CCK chapanga kushtaki polisi
Chama cha Kijamii (CCK) kimesema kinatarajia kulishtaki Jeshi la Polisi mara baada ya kukamilika kwa mpango wa ukusanyaji wa taarifa kuhusu mauaji yaliyofanywa na Polisi huko Songea.

Mwenyekiti wa CCK, Constantine Akitanda alisema jana katika taarifa yake: “Hatua ya kulipandisha jeshi la Polisi kizimbani itakuwa ni tukio la kihistoria katika kuitikia wito wa kutetea haki za wananchi wetu.” Hata hivyo, hakusema ni lini hatua hiyo itachukuliwa.

Alisema chama hicho kimependekeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iingilie kati sakata hilo ili kujua ni kwa namna gani wahusika mbalimbali walivyochangia mauaji hayo.

“Pia Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu achunguzwe kuhusu kauli yake kwamba polisi waliwaua wananchi waliokuwa wakiandamana kuelekea kwenye majengo ya Serikali,” alisema Akitanda.

Akitanda alisema chama hicho pia kinapendekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema kuhojiwa kuhusu matukio ya mauaji ya polisi ambayo yamekuwa yakifanywa mara kwa mara hapa nchini.

shelukindo matatani

VIVA LE TANZANIA
Shellukindo matatani Dar Send to a friend
Saturday, 25 February 2012 08:45

Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo

Elias Msuya na Leone Bahati
MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ametakiwa kuripoti katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ifikapo Machi 7 mwaka huu, ili kusikiliza hukumu ya kesi ya madai inayomkabili.

Shelukindo anadaiwa kushindwa kulipa mkopo aliouchukua kutoka kwenye benki ya Azania mwaka 2005.
Hakimu wa mahakama hiyo, Joyce Minde alisema hukumu ilishatolewa na mahakama hiyo ambayo ilimamuru Shellukindo kulipa deni analodaiwa na benki hiyo, lakini hadi sasa ameshindwa kutekeleza amri hiyo.

“Hiyo kesi siyo ngeni, ni kesi ya madai namba 92 ya mwaka 2005 na ilishatolewa hukumu. Tunachofanya sasa ni kukazia hukumu tu,” alisema Minde na kuongeza:

“Kuna njia mbalimbali za kukaza hukumu kama vile kukamata mali za mdaiwa, mfano nyumba au kufungwa jela.”
Alisema; “Nitasikiliza utetezi wake na nitatoa hukumu kulingana na uzito wake. Kama hauna uzito mahakama itachukua hatua kali, ili alipe deni hilo.”
Hata hivyo, Minde hakuweka wazi kuwa hukumu ya kwanza ilisomwa lini kwa maelezo kuwa, yeye hakuwapo wakati hukumu hiyo ilipotolewa.

Kwa upande wa Benki ya Azania inayomdai Shellukindo, haikuwa tayari kueleza kiasi cha fedha inachomdai wala mwenendo wa kesi hiyo huku wasemaji wa benki hiyo wakielezwa kuwa kwenye vikao kwa muda mrefu.

“Ni kweli hiyo kesi ipo, lakini mimi siyo msemaji. Kwa sasa wasemaji wa benki wako kwenye kikao cha muda mrefu, labda ufuatilie huko huko mahakamani ” alisema mmoja wa watumishi wa benki hiyo anayefanya kazi katika kitengo cha sheria ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Shellukindo ajibu
Alipotakiwa kuzungumzia kesi yake hiyo, Shellukindo alisema hana taarifa kwamba mahakama imemtaka afike mahakamani hapo Machi 7 kusikiliza kesi hiyo.

"Mimi sina taarifa yoyote kwamba natafutwa," alisema Shellukindo akielezea kushangazwa na jinsi jambo hilo linavyopewa umuhimu mkubwa na vyombo vya habari kwa kile alichosema, "We ni mwandishi wa kumi unanipigia kuniulizia juu ya jambo hilo."

Alikiri kuwa ni kweli ana deni analodaiwa na benki hiyo na kwamba, suala hilo siyo la ajabu kwa sababu ni Watanzania wengi wamekopa benki na wanadaiwa hivyo anashangaa kuona yeye kukopa imekuwa ajabu.

Hata hivyo, alitafsiri suala hilo kuwa ni mchezo unaochezwa na maadui zake kisiasa kwa lengo la kumchafua na kushusha heshima yake mbele ya jamii.

Shellukindo alienda mbali akiwatuhumu baadhi ya waandishi wa habari wanaolifuatilia suala hilo kwamba wamehongwa ili kumchafua."Siyo ajabu sasa watakuja wachunguze mimi na mume wangu tuna ndoa au la," alilalamika Shellukindo.
VIVA LE TANZANIA

Barrick kuwekeza zaidi kwenye elimu nchini

INAKUWAJE NDUGU ZANGUNI?

VIVA LE TANZANIA
Hey guys after a long silence now i'm back seriously!!!!!

Tuesday, April 6, 2010

MABADILIKO YA WEAKUU WA WILAYA

VIVA LE TANZANIA
JK AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya nchini kwa kuwahamisha na kuwapangia vituo vipya kama ifuatavyo:-


1. Gishuli M. Mbegesi - Njombe amepangiwa kwenda Kilindi
2. Leonidas T. Gama - Mbeya amepangiwa kwenda Ilala
3. Frank A. Uhaula - Tarime ameoangiwa kwenda Kiteto
4. Bi. Sarah Dumba - Kilindi amepangiwa kwenda Njombe
5. John B. Henjewele - Kiteto amepangiwa kwenda Tarime
6. Rashid M. Ndaile - Chunya amepangiwa kwenda Mkinga
7. Evans Balama - Ilala amepangiwa kwenda Mbeya

8.Florence A. Horombe -Bukombe amepangiwa kwenda Nzega
9. Bi. Zainab Kwikwega -Kasulu amepangiwa kwenda Makete
10. Bi. Hawa Ngh’umbi -Makete amepangiwa kwenda Bukombe
11. Lt. Col. John Mzurikwao -Mpanda amepangiwa kwenda Sumbawanga
12. Bi Betty Machangu -Nzega amepangiwa kwenda Kasulu
13. Dk. Rajab Lutengwe -Ulanga amepangiwa kwenda Mpanda
14. Francis Miti -Tandahimba amepangiwa kwenda Ulanga
15. Deodatus Kinawiro -Mkinga amepangiwa kwenda Chunya

Taarifa ya uteuzi huo iliyosainiwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bw. Aggrey Mwanri imesema pamoja na mabadiliko hayo, Rais Kikwete pia amemteua Bibi Husna Mwilima aliekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Wanawake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba kuchukua nafasi ya Ndugu Francis Miti ambaye anahamia wilaya ya Ulanga.

Aidha, Rais Kikwete ametengua uteuzi wa Bw. Thobias M. Sijabaje ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kutokana na kutosimamia vizuri zoezi la ugawaji wa vocha za pembejeo za kilimo katika wilaya ya Sumbawanga katika msimu wa mwaka 2009/2010.

Mabadiliko haya yanakusudia kuongeza ufanisi wa kazi, kuimarisha utendaji katika wilaya hizo na yanaanza mara moja.


Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S. L. P. 3021
DAR ES SALAAM
Jumanne, Aprili 06, 2010.

HII NI NOMA

VIVA LE TANZANIA
libeneke la eapoti

Asalaam Aleikh,SHISHI

hebu on ajinsi TAA wanavyofanya tuchekwe na wageni pale eapoti ya uwanja wa ndege wa Julius Nyerere... Kuna AC inavuja maji wahusika wapo tuu wanategesha dustbins kukinga maji!!! Jionee mwenyewe taswira ya nchi inavyoharibiwa na wachache wenye dhamana.

MdauHarold E. N.

UCHAGUZI

VIVA LE TANZANIA
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA READING KUFANYIKA TAREHE 25/04/2010
Nakuchukua fursa hii kuwataarifu Watanzania waishio Reading ya kuwa kutakuwa na mkutano mkuu wa kuwachagua viongozi wa jumuiya yetu hapa Reading tarehe 25/04/2010 ,kwa yoyote yule atakayependa kuwania nafasi basi unatakiwa kujaza form iliyopo kwenye kiambanishi na kuirudisha kabla ya tarehe 20/04/2010.
Upatapo ujumbe huu basi mjulishe na mwenzako.Form zirudishe kwenye email ya Jumuiya na kama unamaswali yoyote yale basi usisite kuwasilaina na sisi.

NAFASI ZA KUGOMBEA
NGAZI YA JUU
1:Mwenyekiti
2:Makamu Mwenyekiti
3:Katibu4:Katibu Msaidizi
5:Mtunza Hazina

WAJUMBE
Nafasi Tano za wajumbe
UKUMBI :TUTAWAJULISHA
MUDA:SAA NANE MCHANA(ZINGATIENI MUDA)
TAREHE:25.04.2010
--
Jumuiya Ya Watanzania Reading-UK
http://www.tanzaniaassociation-rea

tsup wadau!!!!!!!!

VIVA LE TANZANIA
wadau naomba radhi sana kwa kutokuwa hewani kwa muda.nipo masomoni uganda kwa sasa.nipo kampala lakini nawahakikishia nitakuwa nawaletea habari kila week end.big up sana onesmo ndenga wa iringa na wadau wooooote kwa ujumla.heri ya pasaka namba yangu ni:+255764272363 au e mail andyl_13@yahoo.com.big up saana.2po pamoko forever

Friday, February 5, 2010

JAMANI

VIVA LE TANZANIA
LESSONS TO LEARN FROM HAITI FOR TANZANIA
floods causing havoc in Kilosa

By Diaspora writer

It is unfortunately , that at the time in the world again in the the western hemisphere and the southern hemisphere. A disaster happened and the rich people of the world are trying to out do each other in bringing proclaimed heroes and philanthropists .

While the world eyes are glued on their Tv sets watching the tragedy unravel before their eyes in Haiti, in Tanzania we are crying our own version of Haiti in a small part of Tanzania , a place called Kilosa .

In both cases lots of property and in lives were lost according to The Kilosa district executive director, Mr Efrem Kalimalwendo.Mr Kalimalwendo said it was not only Kilosa town that had been affected by the floods, as the small town of Kimamba has also been hit hard.
Mkondoa river has burst its banks and water from the river which has changed its course is ravaging Kilosa town and neighbouring villages.I hear that even the new school term was delayed in parts of the region simpy because lots of displaced are living in schools buildings. SOS CHILDREN VILLAGES estimates that around around 28, 000 families have been directly affected.

The difference between Haiti and Kilosa is that the children of Haiti and its friends in the Diaspora have come together to support the country during this hour of need. Did you know that simon Cowell of X factor is organising a Haiti charity song featuring Leona Lewis , Cheryll Cole , Lady Gaga, Boyance , Robbiee William and above all Wycleaf Jean who is originally from Haiti.
In Tanzania , we have big stars, Bands and celebrities like Twanga pepeta, Kanumba ,Lady Jay dee, Ali kiba , Banana Zorro, Fresh Jumbe (I am told he has a live concert in Dar tonight) and so on .Where are they ? Where is their contribution? Cant these guys put their heads together and come up with something? Why not organise a gig or concert to raise money for the displaced in Kilosa? What are they fearing ? Is it the money or logistics or budget?

They have nothing to loose because all they have to do is to make a record which will cost them next to nothing .It costs them nothing because we the public will buy it any way! What we are asking is for them to donate their popularity, fame, time, talent and names and find a place to hold this concert.

Surely Globu ya jamii can help with Matangazo and we will be there!
Let them leave the rest to us to buy the record.

I hear that my music Icon Ali kiba is in the Uk ;Wouldn’t it be a good idea to dedicate one of his shows to the victims in Kilosa?. Surely £1000 dollars could make a great difference.

Lastly, I have nothing against our stars. I actually applaud them for the great cultural contribution they are making to the society. Personally , its Tanzania music that keeps me going when im carrying my Boxes here especially this winter time. My Ipod is only loaded with Bongo Flava.

Tanzania is a revolutionary country , but a true revolution is the revolution of the Human being , for the most important duty that we have is to translate ourselves into a well organised tool able to provide justice and goodness that will light the surrounding darkness.

REMINDER

VIVA LE TANZANIA
Events @Alliance : REMINDER !

This Friday evening from 7PMm:

CONCERT: NORWAY- TANZANIA – ZAMBIA
4 musicians from Norway, 3 from Tanzania and 3 from Zambia will perform together and mix traditional and modern music.
The team performed in Norway last July at the Folk Music Festival.
In partnership with Nota Project :
Promoting inter-Cultural collaboration between
the TASUBa (Bagamoyo College of Arts),
Stavanger School of Culture and University of Stavanger,
Department of Music and Dance in Norway.
In partnership with Tasuba & Nota Project
7pm/ upstairs/ FREE!
-------------------------

NEXT WEEK:
ART EXHIBITION: “Bamboo weaves and straw weaves”
Exhibition organized by the Embassy of China,
as part of the Celebration Activity of Chinese Spring Festival.


Open 8 – 13 February, Mon. to Sat., 10am - 6pm
Exhibition Hall / FREE !
And also:
You are invited for a free concert hosted by Goethe-Institut
on the 6th of Feb at the Russian-Tanzanian Cultural Centre (Sea View) at 8pm.

Goethe-Institut will be hosting two groups at Sauti za Busara Festival 2010:
Joel Sebunjo & Sundiata from Uganda and Thandiswa from South Africa.
To see the dates for the Zanzibar performances please visit our website: www.goethe.de/tanzania
or
KARIBUNI SANA!

Keltouma BOURHIMI
Coordinator of cultural activities /
Coordinatrice des activités culturelles
Alliance Française
Dar es Salaam - Tanzania
Tel : +255 (22) 2131 406
Fax :+255 (22) 2128 266
Mobile AF: 0755 481 374
E-mail : cultural@afdar.com
www.ambafrance-tz.org

BIOGRAPHY OF PROF.JUSTINIAN RWEYEMAMU

VIVA LE TANZANIA
Project: Biography of Prof. Justinian Rweyemamu
Profesa Justinian Rweyemamu

Ninakumbuka vizuri sana jinsi wanazuoni tulivyostuliwa na kifo cha ghafla cha mmoja ya wachumi wakwanza Tanzania, Prof. Justinian Rweyemamu mnamo mwaka 1982, akiwa na umri wa miaka 40.
Katika umri wake mdogo aliweza kufanya mengi kwa kutumia kipaji chake kwa ajili ya nchi yake na nchi maskini duniani. Katika kipindi hicho marehemu alifanikiwa:
1) kupata PhD ya Uchumi (Harvard),
2) kuandika vitabu kadhaa mashuhuri kuhusu historia na muelekeo wa uchumi wa Tanzania,
3) kuwa mhadhiri na mkuu wa idara ya Uchumi wa kwanza mzawa hapa UDSM, 4) kuwa katibu mkuu Wizara ya Mipango,
5) kuwa Mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya Uchumi,
6) Mjumbe wa sekretarieti ya "Committe for Development Planning", Umoja wa Mataifa, n.k.
Alikuwa mcheshi, msikivu, na mwenye upeo wa hali ya juu katika kuchanganua masuala ya Uchumi na Falsafa. Je watanzania, mnamkumbuka msomi huyu?
Nipo katika mchakato wa kuandika biography ya Prof. Rweyemamu, na ningeomba yeyote mwenye kumbukumbu muhimu tuwasiliane kupitia anuani: mfaume.abdalla@gmail.com

kwa wasifu tembelea:
http://en.wikipedia.org/wiki/Justinian_Rweyemamu

asante

VIMWANA WAPYA WA REDDS

VIVA LE TANZANIA
mwali mpya wa redds afichuliwa usiku huu dar
Bosi wa Masoko wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), David Minja akizungumza usiku wa kuamkia leo katika kiota cha maraha cha Savannah Lounge cha Paradise City hotel jijini Dar wakati wa uzinduzi wa chupa mpya ya Redds. Kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Redds Kabula Nshimo.

Kiongozi wa Bendi ya Machozi, Judidh Wambura
‘’Lady JD akiimba na msanii wa baendi hiyo Choniko Furaha

Hashim Lundenga akimmwagia sifa zake mwali
mpya akiwa anakula konozzz na MC wa shughuli Joketi
kilaji cha redds premium lager kimekuja na muonekano mpya kwenye uzinduzi mahususi uliofanyika usiku huu kwenye mnuso wa nguvu ulioandaliwa na TBL kwenye kiota cha maraha cha savannah lounge kilichopo ndani ya hoteli bomba ya Paradise City ghorofa ya tatu ya jengo la benjami william mkapa towers mtaa wa azikiwe avenue jijini dar na kuhudhuriwa na mamia ya wadau ambao wameonesha kufurahia muonekano mpya wa mwali huyu
bosi wa masoko wa TBL David Minja (shoto) akiwa na meneja wa Kilimanjaro lager George Kavishe (kuume) na meneja wa Safari lager Fimbo Butala (pili kuume) na mdau wakifurahia sherehe za kumfichua mwali redds usiku huu katika savannah lounge
Miss Tanzania 2009 Miriam akiwa na wenzie kwenye uzinduzi huo

Lady Jaydee na Machozi band walikuwapo kutumbuiza
meneja wa redds kabula (shoto) akiongoza jive
savannah lounge palikuwa hapatoshi
ankal na mikonozzz walikuwepo na mama wa mitindo asia idarous (kuume) na khadija mwanamboka pamoja na wabunifu mahiri wa kiume
savannah lounge hakika palipendeza
sio chupa tuu hata kopo limekuja kuwashika kivingine....





KUMBUKUMBU YA KAKA MKUBWA

VIVA LE TANZANIA
kumbuka: februrai 6 ni hepibesdei ya kuzaliwa bob marley


bad card
Nabii wa Reggae hayati Robert Nesta Marley aka Bob Marley alizaliwa 6 Feb 1945 kule kijijini St.Ann, kisiwani Jamaika aka jah make yah!
Hakuna asiye jua kuwa Bob ndie super star wa kwanza ktuoka ktk nchi masiki kama zinavyiitwa nchi za dunia ya tatu! super star huyu ambaye jina lake aliwezi kusaulika kwa kazi yake iliyozaa matunda ya kueneza mziki wa reggae dunia,njia ambazo alizotumia ni gitaa, na kanda za kaseti aina C90 ambazo limepenyeza mziki huo katika mipaka ya kila nchi. mziki wake huo wa Reggae ulifika mpaka katika nchi za kiafrika kwa kupitia kanda za kaseti C 90 au C60.

Bob Marley kama leo angekuwa hai basi angesherekea siku ya kuzaliwa.
Je? leo hii tunateknolojia nyingi mbona wanamziki wengi wamekuwa wavivu kutangaza kazi zao? je tujifunze nini kutoka kwa marehemu Bob Marley?(RIP)

KUMBUKUMBU

VIVA LE TANZANIA
KUMBUKUMBU
Hayati Mchungaji
Aaron B.C. Mabondo
Nimevipiga vita vilivyo vizuri,
Mwendo nimeumaliza, Imani
Nimeilinda. 2 Tim 4:7

Leo 04/02/10 ni mwaka mmoja toka Baba yetu mpendwa Mch. Aaron B.C. Mabondo wa Kibaha Picha ya ndege alipotutoka katika mwili. Mioyo yetu ina huzuni kumkosa lakini tunajua siku moja tutamuona Mbinguni.

Hatutamsahau baba yetu kwa malezi ya upendo
wa kiroho na kimwili aliyotupa, tumejifunza mengi kutoka kwake.

Kwa niaba ya familia ya Mabondo tunapenda kuwashukuru watu wote ambao wameendelea kuwa faraja kwetu na hasa kwa mama katika kumtia moyo kwa njia mbalimbali. Mungu awabariki na kuwazidishia upendo huo kwa wengine pia.
tangazo la msiba huu
BOFYA HAPA

TASAF

VIVA LE TANZANIA
TASAF yaunguruma umoja wa mataifa
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Dkt. Servacius Likwalile (shoto)akisisitiza jambo wakati wa mjadala kuhusu uhusiano kati ya ushirikishwaji wa Jamii , utokomezaji wa umaskini na upatikanaji wa ajira zenye hadhi, mjadala huo umefanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York leo. Anayemsikiliza kwa makini ni Waziri wa Masuala ya Jamii na Ajira wa Netherlands, Bw. Donner wengine katika picha ni jopo la walioshiriki mjadala huo.
(picha na habari kwa hisani ya Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa)
"Ushirikishwaji wa wananchi
maskini kupata ajira ni muhimu"
Juhudi za nchi zinazoendelea za kuutokomeza umaskini na upatikaji wa ajira zenye hadhi na tija, hazitaweza kufanikiwa kama wananchi maskini na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi, hawatashirikishwa katika utoaji na upitishaji wa maamuzi yanayohusu mustakabali wao.
Ushauri huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Dkt. Servacius Likwelile, wakati wa majadiliano kuhusu dhana ya uhusiano kati ya ushirikiwaji wa jamii, utokomezaji wa umaskini na upatikanaji wa ajira zenye hadhi.

Majadiliano hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 48 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayohusika na Maendeleo ya Jamii.

Dkt, likwelile ambaye alikuwa mmoja wa wanajopo wanne walioshiriki majadiliano hayo, amewaeleza wajumbe waliokuwa wakifuatilia majadiliano hayo kwamba, kunauhusiano au muuingiliano mkubwa kati ya ushirikishwani wa wananchi na utokomezaji wa umaskini na upatijanaji wa ajira.

“ mafanikio yoyote katika upunguzaji wa umaskini, unategemea sana pamoja na mambo mengine upatikanaji wa fursa kwa watu maskini kupigania haki zao kwa kupitia mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoja na taratibu za kisheria. Inataka ushirikishwaji madhubuti wa jamii hiyo katika shughuli za uendeshaji wa uchumi na hasa zile zenye manufaa kwao”. akabainisha Dkt. Likwalile.
Akaeleza kuwa licha ya juhudi mbalimbali za kitaifa na kimataifa za kuanzisha mipango na sera za kuutokomeza umaskini, takwimu zinaonyesha idadi ya watu wanaoishi katika umaskini imeongezeka kutoka 190 milioni mwaka 1990 hadi milioni 380 mwaka 2005.

Wengine walioshiriki mjadala huo ni Dkt. Beatriz Merino kutoka Peru, Bw. J. Piet Hein Donner Waziri wa Wizara ya Masuala ya Jamii na Ajira kutoka Netherlands na Profesa Vojtech Tkae ambaye ni mshauri wa Waziri wa Ajira , Masuala ya Jamii na Familia nchini Slovakia.
Kama hiyo haitoshi Dkt Likwelile anaongeza kuwa unyimwaji wa haki za jamii ni mkubwa, kutengwa kwa watu maskini ni jambo la kawaida na ukosefu wa huduma za msingi za jamii ni jambo la kawaida katika nchi nyingi hasa barani Afrika.

Akasema ni muhimu pia kwamba haki za kijamii na za kisiasa zikajielekeza zaidi katika uwezeshwaji wa watu maskini na sit u katika kudai haki zao za kiuchumi na kijamii lakini pia kudai uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma bora za jamii, sera zinazowajali wanyonge na uwazi katika mchakato mzima wa ushiriki wao.

Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TASAF akaeleza kuwa ,Tanzania kupitia mfuko huo imejitahidi sana kuwashirikisha wananchi maskini na wanaoishi katika mazingira magumu, kushiriki na kupitisha maamuzi ya miradi inayolenga kuwaondolea umasikini na kuwapatia ajira.
Anatoa mfano kwa kusema,TASAF huwapa fursa wananchi katika ngazi ya kijiji au eneo wanaloishi kuchagua ni aina gani ya mradi wa maendeleo wanaoutaka, ushiriki wao katika utekelezaji wa mradi huo, udhibiti na matumizi ya fedha za mradi huo pamoja na kuangalia ni familia gani iliyokatika mazingira magumu inayostahili kupata ajira kupitia mradi huo.

“Tanzania kama zilivyo nchi nyingi za Afrika, asilimia 34 ya wananchi wake wanaishi chini ya mstari wa umaskini wa upatikanaji wa huduma za msingi, huku asilimia 18 wakiwa katika umaskini wa upatikanaji wa chakula. Kwa hiyo mifuko ya jamii kama tasaf na mingineyo pamoja na mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini ( Mkukuta) malengo yake ni kutoa fursa za ushirikishwaji wa jamii” akasema.

Akichangia kuhusu mweleko wa baadaye katika dhana hiyo ya ushirikishwaji wa jamii na uhusiano wake katika kuutokomeza umaskini na upatikanaji wa ajira zenye hadhi, Dkt likwalile anasema juhudi za makusudi pamoja na utashi wa kisiasa kutoka kwa makundi mabalimbali ya viongozi wa kisiasa, taasisi za kijamii, washiriki wa maendeleo zinatakiwa katika kuhakikisha kuwa mwananchi maskini anashiri katika mambo yanayo mhusu.

Aidha anasema kuwa kuna kila sababu ya kutilia mkazo wa upatikanaji wa elimu lakini siyo bora elimu bali elimu yenye ubora ambayo itawajenga uwezo wa ushiriki katika utoaji wa maamuzi.
Uwepo wa mipango ya muda mrefu, ya ujenzi wa uwezeshwaji wa wananchi maskini na wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka ngazi ya chini ni jambo analolitilia mkazo. Huku akitaka kufanyika kwa tathimini ya wapi nchi husika imefanya vizuri na wapi imekosea kwa maana ya sera, mikakati na michakato mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Anasisitiza pia haja ya kutadhimini ushirikiano kati ya serikali, taasisi za kijamii, sekta binafsi na mataifa hisani katika utekelezaji wa ajenda nzima ya ushirikishwaji wa jamii.

Akaongeza kuwa ubaguzi wa jamii wa aina yoyote ile unachangia ukuaji wa umaskini kwa vile wananchi maskini na wanaoishi katika mazingira hatarishi wananyimwa haki na fursa ya kupata ajira zinazojitokeza, ajira ambazo zinaweza kuwa chanzo kikubwa cha wao kuondokana na umaskini na mazingira hatarishi.

MAMBO YA TBC

VIVA LE TANZANIA
TBC yaandaa kitimtim cha uchaguzi
mwendeshaji wa kipindi kipya cha TV katika TBC1 Maria Shaba akiongea na mwakilishi toka ubalozi wa Uingereza nchini pamoja na prodyuza Dk. Martin Mhando na msanii Vitalis Maembe, Rose Haji wa MISA-Tan na Mh. John Mnyika wa CHADEMA baada ya kukamilisha kurekodi sehemu ya kwanza ya kipindi cha 'Kitimtim' kitachoanza kurushwa hivi karibunik ikiwa ni kuamsha na kuelimisha wananchi kuhusu wajibu na haki katika uchaguzi mkuu. Fungua dimba ni mada ya Ushiriki na utendaji wa vyombo vya habari katika uchaguzi mkuu

Wednesday, January 27, 2010

DOGOSHISHIS(LIMBE) SPECIAL THANKS!!!

WADAU WOTE KWA UJUMLA NAWASHUKURUNI SANA KWA KUWA NAMI KWA TANGU NIANZISHE LIBENEKE HILI LA BLOGU.AMANI KWENU ONESMO LUAMBO(GUM2)UKIWA PANDE ZA IRINGA KAZA BUTI KAKA WEWE NI WA MCHEPUO WA SAYANZI NAKUSHUKURU SANA KWA KUWA NAMI BEGA KWA BEGA AMANI KWAKO.WADAU ASANTENI SANA TUENDELEE KUWA PAMOJA.I LOVE U ALL!!

YOURS,
DOGOSHISHI E.

ENENDENI ZANZIBAR!!

VIVA LE TANZANIA
zanzibar welcomes you all

The tourism industry is no doubt aware that Zanzibar has not been supplied with mains electricity power since before Christmas. This is due to a fault on the power cable line between the island of Zanzibar and the mainland, which is being rectified, with normal power expected to resume mid February.


In the meantime we would like to assure operators and visitors to Zanzibar that the island is well equipped to deal with this temporary situation as power outages are commonplace and generator backup is provided in all hotels and resorts.


Therefore all services including tourism, communication and transportation continue to function with no significant or noticeable disruption. In addition to this, ZATI would like to assure all visitors heading to Zanzibar for Sauti za Busara Music Festival commencing 11th of February that Zanzibar Commission for Tourism, and Zanzibar Association Tourism Investors, are both giving a clear message that Zanzibar is open for “business as usual”


We are confident that Zanzibar is safe for visitors. The longer the power outage has gone on, the more Zanzibaris have been getting back to “business as usual”. All hotels, restaurants and businesses in Zanzibar Town are open and many streets have lighting. Local people are preferring to go out in the evenings – especially in the area of night food market at Forodhani Gardens. All indications are that our local and perhaps regional audiences shall be greater than ever.


The island of Zanzibar welcomes visitors and continues to be the same peaceful and secure environment that we are proud to be part of. Thank you for continuing to support us. We will issue an update as soon as mains power is back on line.


On behalf of

Zanzibar Association of Tourism Investors

Simai M Said

CHAIRMAN

ZATI

WADAI URAIA UGIRIKI

VIVA LE TANZA
JANA TAREHE 26/01/2010,WAGENI WALIAANDAMA NDANI YA AHENS KUDAI HAKI ZAO,KWA WATOTO WALIOZALIWA HAPA NA WAAMIAJI KUTOKA NCHI TOFAUTI ILI WATAMBULIWE KAMA RAIA WA HAPA NA WAZAZI AU WAGENI WALIOKUWA HAPA NAO WAPEWE HAKI ZAO IKIWA URAIA NA MAMBO MENGINE,JUMUHIYA YA WATANZANIA ATHENS-GREECE ILISHIRIKI KIKAMILIFU MAANDAMANO HAYO,ILIONGOZWA NA KAYU KAMA KATIBU MKUU WA JUMUIYA (PICHANI) PAMOJA NA MSAIDIZI WAKE BWANA MUNGI.
NIA

CHANGIA MAAFA

VIVA LE TANZANIA
Vodacom Tanzania inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wasamaria wema ambao wamechangia harambee ya kusaidia ndugu zetu walioathirika na maafa sehemu mbalimbali nchini ikiwemo kilosa kulikokumbwa na mafuriko makubwa mwaka huu. Inasema asante sana kwa moyo wa uzalendo.
Kwa kuwa tatizo bado lipo, michango hiyo ya harambee ya maafa kupitia kampeni ya 'Vodafone Red Alert' inadelea kila siku na kupokewa ambapo unatuma kwa sms neno 'MAAFA' kwenda namba 15599 nawe utakuwa umechangia bila tatizo. Shime wadau kutoa ni moyo....

WANAJESHI WANAOSHUKIWA MAUAJI WAFIKISHWA KIZIMBANI!

VIVA LE TA
BREKING NYUUUUZZZZ: WANAJESHI WANAOTUHUMIWA KUMUUA SWETU WATINGA MAHAKAMANI KISUTU LEO
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya marehemu Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi wakisindikizwa kuelekea chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar mchana huu.
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira, marehemu, Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi wakiwa katika chumba cha Mahakama leo.
Ndugu wa marehemu, Swetu Fundikira wakiwa nje ya mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi ya mauaji ya ndugu yao ikiwa inaendeklea.
Kushoto ni Nzwala Fundikira na kulia ni Ismail Fundikira.


Washtakiwa wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Geni Vitus Dudu na mashtaka yameendeshwa na wakili wa serikali Monica Mbogo aliyekuwa akisaidiwa na Beatrice Mpangala
Mh. Dudu aliwaeleza washitakiwa hao kwamba kwa mujibu wa kosa linalowakabili hawatakiwi kujibu chochote na kwamba kosa hilo halina dhamana kwa sababu hiyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na kuairisha kesi hiyo Februali 10 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa. Akaamuru washitakiwa wote wamepelekwe rumande.
Ndugu wa marehemu Swetu walikuwepo mahakamani na kusikiliza kesi kwa utulivu, huku wakisema wana imani kwamba haki itatendeka.

Swetu Fundikira alifariki dunia Jumapili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambakoo alilazwa toja Ijumaa usiku baada ya kupigwa sana na wanajeshi watatu, wawili wakituhumiwa kuwa ni hao pichani na mwingine wa tatu haijulikani alipo na msako unaendelea.

Marehemu Swetu alizikwa jana kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar. Kifo chake kimezua zogo kubwa miongoni mwa wananchi ambao wanadai uongozi wa majeshi yote ya ulinzi na usalama uwe wakali kuhakikisha askari wachache wenye mtindo wa nidhamu hawapewi nafasi ya kuchafua majina mazuri waliyo nayo pamoja na ushirikiano mwema kati yao na jamii.

NZANIA

Thursday, December 10, 2009

MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI

VIVA LE TANZANIA
JK aongoza baraza la mawaziri
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha
baraza la mawaziri ikulu jijini Dar leo asubuhi

JK NA SIMBA WA VITA!!

VIVA LE TANZANIA
JK ateta na simba wa vita
JK akiongea na Mzee Rashid Mfaume Kawawa katika viwanja vya ikulu jana usiku wakati wa hafla maalum ya kusherehekea miaka 48 ya Uhuru

KUMBUKUMBU

VIVA LE TANZANIA
REMEMBRANCE
The Late DEUSDEDIT HENRY MAEMBE NDENJE

04 March 1973 – 11 December 2004


Brother, it's been five years since death snatched you away from us leaving that emptiness in our hearts. You heard the call of your Master and Savior and responded to it. We love you but The Almighty God Who gave you to us thought the need to take you away from us. We cannot question his works, but trust that He will keep you until that day when we all shall meet you again.

For and on behalf of Ndenje’s family, we want to extend our heartfelt thanks and appreciation to all of you who stood by us and supported us during that time of bereavement. We could not have done it all alone without your help. We still appreciate your support, prayers, thoughts etc. that we received.

From: Francis Ndenje
For the Family

UZINDUZI

VIVA LE TANZANIA
uzinduzi wa ripoti ya taifa ya hesabu sekta ya afya
Mganga Mkuu wa serikali Dk. Deo Mutasiwa akizindua rasmi ripoti ya Taifa ya hesabu katika sekta ya Afya (NHA) ya mwaka 2002/3 na 2005/6 ikionyesha matumizi katika magonjwa ya Malaria, Kifua Kikuu, Ukimwi na katika Afya ya mama na motto leo jijini Dar.
Mganga Mkuu wa serikali Dkt. Deo Mutasiwa akimkabidhi mwakilishi wa shirika la Ushirikiano na Maendeleo la Uswiswi (Swiss Agency for Development and Cooperation) Bw. Jacques Mader ripoti ya Taifa ya hesabu katika sekta ya Afya (NHA) ya mwaka 2002/3 na 2005/6 ya matumizi katika magonjwa ya Malaria, Kifua Kikuu, Ukimwi na katika Afya ya mama na mtoto mara baada ya uzinduzi leo jijini Dar

Mganga Mkuu wa serikali Dkt. Deo Mutasiwa akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya nchini kutoka serikalini, Taasisi mbalimbali na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya hesabu katika sekta ya Afya (NHA) ya mwaka 2002/3 na 2005/6 ikionyesha matumizi katika magonjwa ya Malaria, Kifua Kikuu, Ukimwi na katika Afya ya mama na mtoto.